TITANIC“MELI YA TITANIC | MAMBO 7 YAKUSHANGAZA AMBAYO HAYAKUWAHI KUSIMULIWA” NA IBRAHIM NUHU-

       TITANIC
“MELI YA TITANIC | MAMBO 7 YAKUSHANGAZA AMBAYO HAYAKUWAHI KUSIMULIWA”
Historia yake ni ya ajabu kuliko meli zote,sio kwasababu ya tajiri wa dunia wakipindi hicho bwana  John Jacob Astor kuwa mmoja kati ya wahanga waliopoteza uhai , lakini kwasababu ya kile ambacho hakitosahaulika
Mwanzoni ilizua gumzo duniani kote… kwa ufahari,uzuri,ukubwa kuliko meli zote ulimwenguni pamoja na mapinduzi makubwa katika ufanisi wa wanadamu

Lakini punde ikapelekea huzuni na machungu ambayo ni kazi kuyaelezea kwa maneno ya kawaida,ajali ikaacha  mafumbo yasiyo na majibu hadi hivi leo

Siku meli ya Titanic ilipozama chini ya mawimbi ya bahari ya antlantic pamoja na roho za watu zaidi ya 1500 itaendelea kubaki kumbukumbu ya majonzi katika Historia ya wanadamu
Na pamoja ya miaka 108 kupita , bado hadi hivi leo wanasayansi , wachunguzi na wasanii  wanaendelea kufuatilia tukio la masaa mawili na dakika 40 lililobeba mikasa zaidi ya 2208

Nina imani ni mengi ya ajabu bado huyafahamu juu ya tukio hilo ,na leo nimekuandalia mambo 7 ya ajabu yasiyosahaulika kuhusu meli ya titanic ambayo yatakushangaza









KULIKUWA NA UWEZEKANO WA WATU WOTE KUOKOLEWA
Mwezi wa nne wa tarehe 14 mwaka 1912, saa ilisoma saa 5 na dakika 40 za usiku
Meli kubwa ya Titanic ikagonga mwamba wa barafu kwa ubavu wake wa kulia ,
 na kujisababishia matobo makubwa yaliyoanza kuingiza  maji kwa nguvu ndani ya meli hiyo

Wakati janga hilo lilipokuwa likitokea Nahodha wa meli ya Titanic alijitahidi sana kupiga simu kwenye meli ya SS carifornia waliyogundua ilikuwa jirani sana na mahali walipo lakini hakukuwa na majibu .
mtu pekee aliyehusika na kupokea simu katika meli ya SS California alikuwa amelala ,yaani kama zingekuwa ni nyakati za mchana na simu hiyo ingepokelewa upesi basi hivi leo tukio hilo la kuhuzunisha lisingeongelewa kabisa
Nahodha  wa Titanic akajihisi kupagawa baada ya kujaribu kila njia kuwajurisha watu waliokuwa kwenye meli ya SS California
inasemekana wafanyakazi wa SS california waliona mwanga wa baruti iliyopigwa kuashiria uhitaji wa msaada ,nao wakaenda upesi kumwambia Nahodha wa Meli yao,lakini Nahodha huyo alichukulia poa tu,nakutaka asisumbuliwe katika nyakati hizo .
inasemekana hakujua kama meli hiyo ilikuwa ni meli ya abiria au labda zilikuwa ni akili za usingizi , na kwasababu ya baridi kali lililokuwepo labda nahodha wa meli hiyo alikuwa na mtu aliyeshindwa kumuacha ndani humo.
 baada ya masaa machache kupita, katika mida ya wanga yaani saa 8 za usiku meli ya Titanic ikakatika Katikati na kujigawa vipande viwili
na baada ya dakika chache,   Meli ikazama na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1500
Watafiti wanadai kuwa meli ya SS California ilikuwa na uwezo wa kuokoa maisha ya watu wote waliokufa katika meli ya Titanic .
  hadi hivi leo meli ya SS California inakumbukwa kwa tukio hilo la kizembe huku lawama zikimzonga Nahodha wa meli ya SS California hadi anaingia kaburini.





KULIKUA NA RIWAYA ZILIZOELEZEA  AJALI YA TITANIC HATA KABLA MELI HIYO KUTENGENEZWA.
Mwaka 1886 mwandishi  kutokea british aitwae William T stead ,aliandika kitabu alichokiita “from the old world to the new world “ yaani kutokea ulimwengu wa zamani kuelekea mpya. 
Kwenye kitabu hicho aliongelea meli kubwa sana iliyozama kaskazini mwa bahari ya antlantic nakusababisha vifo vya watu wengi baada ya kugonga mwamba wa barafu, na cha ajabu zaidi jina la Nahodha alilotumia katika kitabu chake lilifanana na jina la Nahodha wa Meli ya Titanic
Pia mwaka 1898 yaani miaka 14 kabla ya meli ya Titanic kuzama, mwandishi mwingine aitwae  Morgan Robertson aliandika riwaya aliyoiota futility. Riwaya hiyo iliongelea meli kubwa aliyoiitaa titan  jina lililofanana na meli halisia ya Titanic , kwenye hadithi ilielezewa meli hiyo kutokuwa na maboti ya kutosha kama ilivyokuwa kwenye meli ya Titanic ,pia meli zote mbili zilipewa jina la unsikable yaani Meli isiyozama, na kama haitoshi Meli ya Titan kwenye riwaya ya bwana Morgan  ilizama mwezi wa nne kama ilivyozama meli ya Titanic,
., inasemekana kitabu cha Morgan Robertson kilitabiri tukio lote la kuzama kwa meli ya Titanic kiasi kwamba akakumbwa na shutuma za uchawi na wengine wakiamini yeye ndiye aliyesababisha janga hilo, hata hivyo Morgani Robertson alijibu shutuma zile kwa kudai kuwa ufanano huo  ulitokana na kujua kwake mambo mengi.



WANAMZIKI WALITUMBUIZA HADI DAKIKA YA MWISHO

Kulikuwa na matukio mengi ya kishujaa yaliyofanyika usiku huo wa kihistoria,bila kusahau wahandisi waliojitoa kafara kuendelea kufanya kazi kuhakikisha meli hiyo haizami wala umeme haukatiki lakini hakukua na tukio lililogusa mioyo ya watu wengi kama tukio la bend ya muziki lililoongozwa na bwana  Wallance Hartley .
Inasemekana wakati meli hiyo ilipokuwa ikizidi kuzama majini kwa kila dakika,watu wengi walikuwa wakijaribu kuingia katika maboti machache yaliyokuwepo ili kuokoa maisha yao…
Lakini wanamuziki 8 waliokuwa wakitumbuiza waliendelea kutumbuiza kwa ajili ya kuondoa hofu na kupoza mioyo ya watu waliopaniki..
Inasemekana kuna baadhi ya watu waligoma kupanda maboti na kubaki wakikonga nyoyo zao wakisikiliza nyimbo,  zilizopigwa kiufanisi usiokuwa wa kawaida..
Watu waliopona walidai kusikia nyimbo iliyotumbuizwa  kabla ya meli kuzama na kupotea baharini  , kilikuwa kibao kilichopendwa kwenye makanisa mengi kiitwacho “Neerer,My God to thee” yaani jirani na mola wangu.
Wanamuziki hawa wote walifariki siku hiyo lakini hadi hivi leo wanakumbukwa kama mashujaa kwa jambo walilolifanya.




Pombe yaokoa maisha ya Charles Joughin
Kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu, Pombe imeonekana kuwa ya muhimu kuliko vitu vyote katika ajali ya Titanic, labda hata abiria wote wangelewa usiku huo basi vifo vingekuwa vichache au visingekuwepo kabisa.
Kati ya visa zaidi ya 2208 vilivyotokea katika usiku huo wa kihistoria ,kisa kilichoduwaza watu wengi ni kisa cha mpishi wa meli ya Titanic,
Mpishi huyo Aliweza kukaa kwa takribani masaa matatu kwenye maji yenye baridi lisilo la kawaida ambalo kwa watu wengine walikufa ndani ya dakika chache.
Kabla ya ajali hiyo kutokea bwana Charles Joughin alikuwa amelala,meli ilipogonga mwamba wa barafu na kupelekea mtikisiko mkubwa , Bwana Charles  aliyekuwa katika mapumziko baada ya kujichokea akaamka…
baada ya kugundua kuwa hali ilikuwa ni tete,na watu walikuwa wakiamishiwa kwenye maboti ili kuokoa maisha yao, bwana Charles Joughin akawashangaa watu wale kukimbia janga la meli kuzama na kusahau janga la njaa ambalo labda lingewakuta wakiwa kwenye maboti.
Basi mpishi Yule akahakikisha kila boti lilikuwa likipata chakula. 
Wakati huo Meli ya Titanic iliendelea kudidimia kwenye maji yenye ubaridi mkali zaidi ya friji..kwa nukuu za ofisa msaidizi wa meli ya Titanic aitwaye Lightoller alisema “kugusa maji ya bahari ya atlantic ilikuwa ni sawa na kuchomwa visu elfu moja mwilini”
Sauti za majonzi na vilio vya watu viliendelea kusikika, Bwana Charles Joughin aligundua kuwa hakuwa na mahali pakukaa kwenye maboti ya kuokolea  , basi akarudi  chumbani kwake nakuchomoa kinywaji aina ya whiskey,..mpishi huyo alikunywa na kujigalagaza…
Maamuzi aliyochukua yalitofautiana na watu wote lakini yalikuwa maamuzi pekee yaliyookoa maisha yake.
Baada ya muda kidogo umeme ukakatika nakusababisha watu wote kupoteza matumaini..kasoro bwana Charles ambaye hakua amepaniki kwasababu pombe ilimpa ujasiri usio wa kawada.
meli ya titanic ikakatika na kujigawa Katikati,na yote ikazama ndani ya bahari ya atlantic ,ikiwa na maelfu ya watu pamoja na bwana Charles Joughin.
Kwa watu wengi kuingia kwenye maji hayo yenye kiwango cha baridi  kali 
Wakajikuta wakipata mshtuko wa ghafla na kupoteza uhai, wanasayansi wanadai  vifo vingi vilitokana na mshtuko huo uliosababishwa na baridi  pamoja na hali ya kupanic iliyopelekea hata mafundi wa kuogelea kuzama, na waliojitahidi kuogelea walikufa kwasababu ya baridi kali lililotafuna miili yao ndani ya dakika chache
Lakini hali ilikuwa ya tofauti kwa bwana Charles Joughin , mtaalamu wa kuogelea aliyelewa tilalila,aliweza kukaa zaidi ya masaa matatu kwenye maji ya barafu,
katika kiza kizito cha atlantic, ni makelele ya vilio vya watu waliokuwa wakifa ndiyo yaliyokuwa yakisika,bwana Joughin alikaa kwenye maji hayo hadi jua lilipoanza kuchomoza,ndipo akaogelea kusogelea boti aliloliona ,watu wakamshangaa walipomuona,na japokuwa hakukuwa na nafasi lakini wakamsaidia kwa kumshika mkono huku Miguu yake ikiwa ndani ya maji hadi msaada wa meli ya Caparthia ulipofika…
Bwana Charles Joughin anakumbukwa kama mlevi aliyelishinda janga kubwa zaidi katika karne ya 20.



WANAUME KUVAA NGUO ZA KIKE ILI KUPATA NAFASI KWENYE BOTI
Ajali ya meli ya Titanic haikuacha kumbukumbu za majonzi peke ake bali na vihoja vilivyoacha watu midomo wazi,huku wengine wakikumbukwa kwa ushujaa,wapo waliopigania kupona hata kama wakikumbukwa katika kashfa mbaya na kuathiri maisha yao yote.
Jua lilipochomoza na wakati meli ya Carpathia inakaribia eneo ilipozama meli ya Titanic, wanaume wengi wakaonekana katika mavazi ya kike huku wakiwa wametulia kama akili zao haziko sawa, kihoja hiki kilisababisha ndoa kuvunjika na wengine kama masabumi Hosono kupoteza ajira yake  pamoja na heshima nchini kwake huku akitangazwa nchi nzima kama msaliti wa tamaduni na imani zao walizozitukuza.
Ni nini kilitokea katika masaa mawili hayo na dakika 40 za ajali ya kifo , na kusababisha baadhi ya wanaume kuwa katika muonekano wa kike…
Kuelewa kisa hiki inabidi turudi nyuma kidogo
Meli ya Titanic  ilikuwa na uwezo wa kubeba watu 3547, na kwa bahati nzuri siku hiyo ya safari kulikuwa na watu 2224 .
Mpango ulioandaliwa na wataalamu ni kuwa Meli hiyo kuwa na maboti ya dharura  48,lakini
Idadi ikapunguzwa na Mmiliki wa meli hiyo akitaka idadi ya maboti kupungua hadi 20,kwasababu aliona maboti mengi yangeziba nafasi na kuzuia muonekano mzuri wa bahari ya atlantic.
Baada ya ajali kutokea nafasi ya upendeleo ilikuwa kwa wanawake na watoto, hivyo wanaume wengine wakavaa mavazi ya kike nakujifanya wanawake ili wapate nafasi katika maboti.
Mwaka 1916 , yaani miaka minne baada ya ajali ya Titanic,abiria mashuhuri aitwaye Dickson akaachana na mke  wake,baada ya mke wake kushindwa kuvumilia kashfa aliyokuwa akishutumiwa mme wake ya kujifanya mwanamke ili apone, 
kashfa hiyo iliwazonga baadhi ya wanaume waliosemekana kuvaa mavazi ya kike pamoja na kuigiza kama wanawake, lakini aliyeathirika zaidi na kashfa hiyo alikuwa bwana Masabumi Hosono, raia wakijapan pekee aliyekuepo kwenye meli ya Titanic.
Kwanza baada ya ajali alipata umaarufu mkubwa nchini marekani na kuhojiwa na vyombo vya habari tofauti huku akipewa jina la “the lucky Japanese boy”, kwani alikuwa mjapani pekee katika watu 700 walioponyeka katika janga hilo la kutisha.

Lakini habari ya wanaume waliovaa nguo za kike ilipofika japan,bwana Masabumi Hosono akajuta kupona kwenye ajali ya Titanic, 
bwana Masabumi alionekana kama mtu aliyeidharirisha nchi ya Japan kwa kushindwa kufa kiume kama tamaduni zao zilivyo, Masabumi akapoteza ajira aliyokuwa nayo Mwanzoni , na kujikuta akizongwa na chuki,dharau ,kutengwa pamoja na kashfa ya aibu hadi alipokufa.

MTU ALIYESABABISHA AJALI YA TITANIC.
Meli kubwa ilizama kwasababu ya kitu kidogo kilichosahaulika katika mifuko ya bwana David Blair.
David Blair alikuwa ofisa wa meli ya Titanic,kabla ya meli hiyo kuanza safari,bwana David blair akaondoka kwa dharura na nafasi yake ikashikiliwa na mtu mwingine, baada ya ajali ya Titanic kutokea wengi walimuona kama mtu mwenye bahati duniani  lakini yeye alikuwa na huzuni kubwa kwani aliujua ukweli ,kuwa yeye ndiye aliyesababisha ajali ya Titanic,na kama angekuwepo ajali hiyo ingezuilika…
Miaka 108 iliyopita katika usafiri wa meli,wafanyakazi wa meli walitumia darubini kutazama kama kuna hatari yoyote mbele yao.
Lakini cha ajabu ,katika safari ya meli ya Titanic ,wafanyakazi wanaohusika na kazi ya kuangalia hawakuweza kuchukua darubini mahali zinapoifadhiwa  kwani bwana David Blair ndiye aliyokuwa na funguo zilizofungia Darubini hizo.
Kwakuwa bwana David Blair aliondoka akiwa na haraka sana,akasahau kukabidhi funguo za darubini.
Watafiti wanadai kama darubini ingekuwepo basi mwamba wa barafu ungeonekana mapema sana ,na ajali isingetokea.
bila darubini,meli ya Titanic ilikuwa kama kipofu anaekimbia Katikati ya barabara yenye visiki na mashimo.
Bwana Frederick fleet na Reginald lee ndio waliotegemewa kutazama kama kulikuwa na hatari yoyote mbele yao,na kwakuwa walikuwa wakitumia macho tu hawakuweza kuona mbali kwenye kiza kizito cha bahari ya atlantic.
Inasemekana ikiwa bado kama sekunde 37 kuufikia mwamba mkubwa wa barafu ndipo bwana Frederick fleet akabwatuka kama mtu aliyekurupuka usingizini
“iceberg,rigjt ahead”…akimaanisha mwamba wa barafu upo mbele , na ndipo harakati za kujiokoa zilipoanza ambazo hazikuzaa matunda na meli ya Titanic ikajikuta ikibamiza vibaya mwamba huo mgumu wa barafu.
Frederick Fleet alikuwa mmoja kati ya abiria waliopona,alibeba lawama nyingi kwa kuonekana mzembe .
Mwaka 1965 akajiua mwenyewe baada ya kifo cha mke wake,na katika kaburi lake zilikutwa darubini mbili pamoja na ujumbe uliosema “samahani kwa kuchelewa kuzileta darabuni“
Kuna watu wanaamini mtu huyo asiyejulikana alikuwa bwana David Blair,aliyeishi maisha yake na majuto mengi
Mwaka 2010,funguo iliyosababisha ajali ya Titanic, ikauzwa kwa dola za kimarekani laki 1.30elfu ambayo ni zaidi ya milioni 300 za kitanzania;



Ndugu zangu visa vilivyotokea kwenye meli ya Titanic vinatosha kuandika vitabu zaidi ya elfu moja lakini kwa leo namalizia na kisa cha cha mapenzi kilichogusa mioyo ya watu wengi ulimwenguni

UPENDO WA KWELI….
Waswahili wanasema,mapenzi upofu,mapenzi uchizi ,hili linatokana na maamuzi yasiyo ya kibinafsi wanayoyaamua watu kwasababu yakupenda…
Katika ajali ya meli ya titanic,yapo matukio yatakayobaki kukumbukwa kama upendo wa kweli katika historia. Katika meli hiyo kulikuwa na wapendanao 26 waliokuwa wakisheherekea fungate yao , ikiwemo tajiri aliyesemekana alikuwa tajiri wa dunia katika kipindi hicho bwana  John Jacob Astor, lakini matukio yaliyothibitisha upendo wa dhati hayakutokea kwa wapendanao hao, bali kwa wanandoa waliodumu kwenye ndoa kwa  miaka 41.  bwana Isidor na mkewe Ida Straus
Kama umetazama muvi ya Titanic,ambayo waswahili wengi tunaiita titanike ,na kama unakumbuka wakati kate Winslet alipoacha nafasi yake kwenye boti ili kufa pamoja na Leornard DiCaprio  basi wazo la igizo hilo lililogharimu zaidi ya gharama zilizotumika kutengenezea meli ya Titanic limetoka kwenye kisa hiki, cha wapendanao..
Isidor na Ida  walitoka ufaransa kwenye mapumziko na kuwa moja kati ya abiria wanaoelekea marekani,ajali ya Titanic ilipotokea,wote kwa pamoja wakawaishwa kwenye maboti kutokana na hadhi walizokuwa nazo…ikumbukwe kuwa boti zilikuwa ni chache sana,kwasababu mmiliki wa meli ya Titanic aliamini kuwa meli hiyo haiwezi kuzama ila matumizi ya maboti mengi yanaeza haribu muonekano wa meli.waswahili husema kipya kinyemi.
Hakukuwa na uwezekano wakupakia kila mtu kwenye maboti,nafasi za upendeleo zilikuwa kwa bahadhi ya wanawake,watoto  na watu wenye hadhi ikiwemo bwana Isidor na mkewe.
Hata hivo millionaire Isidor alipoona watoto wengi pamoja na wanawake wakikosa nafasi akakataa kupanda boti na kutaka nafasi yake apewe mwanamke au mtoto .
Mke wa Isidor aliyekuwa ameshajipatia nafasi katika boti akashuka baada ya mme wake kufanya maamuzi yale, japokuwa Isidor alimlazimu Ida abakie kwenye boti lakini kwa nukuu za abiria inasemekana Ida alimwambia Isidor kuwa “nafasi yangu ipo ulipo,nimeishi na wewe na kukupenda,basi nitakufa na wewe”
Wanandoa wale walishikana pamoja huku wakiwa kimya na kufutana machozi ya uchungu huku bahari ya atlantic ikimeza miili yao.
 kwakuwa upendo wao Ulikuwa wa dhati basi na historia haitowasahau.
Hatahivyo hakuwa Ida peke yake aliyetoka kwenye boti kwa ajili ya mme wake, pia kulikuwa na mwanamama anayekumbukwa kwa jina la Ann Elizabeth Isham
Kama wewe ni mpenzi wa filamu za kimarekani basi utakuwa si mgeni na tukio la mtu kurudi mahali pa hatari kwa ajili ya mbwa wake.
Mwanamama huyu alipoingia kwenye boti akakumbuka kuwa alimsahau mbwa wake aitwaye “Great Dane” basi akakimbia upesi na kurudi kwenye meli na hapo hakuonekana tena akirudi hadi baadae  mwili wake ulipatikana akiwa amemkumbatia mbwa .

Kwa leo tunaishia hapo, asante kwa kutazama hadi mwisho wa video hii , tafadhari subscribe ,share na comment katika channel hii ili  usipitwe na mazuri zaidi yajayo.



.

Maoni