Scene 1
(akiwa sebureni na
wazazi wake,mazoea alitazama simu yake ya kiganjani uku akitabasamu,alikua
amehama kimawazo ,akihangaika kujibu kila ujumbe uliofika katika simu yake)
(Bi.masinde ambaye
ndiye mama yake mazoea alikua amekasirishwa na tabia aliyokuwa akiionyesha mazoea…baada
ya kumuita kwa kipindi kirefu bila ya kupata majibu yoyote .
Bi masinde::we
mazoea!!!,
(mazoea akashituka kama mtu aliyetoka usingizini,nakuanza
kuwatazama wazazi wake kwa mshangao
Mazoea:naam baba.
Bi.masinde: siyo baba
yako!!!, ni mimi ndiyo nakuita(kwa ukali),yani watoto wa siku hizi!!,
(bi masinde alivuta
pumzi kidogo,ili aweze kuongea kwa utaratibu)
Bwana masinde:ngoja
niwaache kidogo muongee
Bi masinde: mume wangu
unaenda wapi?, ili swala hutakiwi kulitazama kwa jicho la upande kabisa!,sote
tunahusika na hili swala
Bwana masinde:ninaelewa
vizuri mke wangu ila kuna kitu kimetokea kazini inabidi nifike
(bwana masinde aliinuka
kitini nakuondoka,bi masinde hakupendezwa na jibu la mume wake, akarudi
kumtazama mazoea ,nakumkuta akitabasamu huku akiitazama simu yake ya kiganjani)
Bi masinde: mwana
mwenye hekima humfurahisha babaye bali mwana mpumbavu ni mzigo wa
mamaye,nimeamini!
(mazoea aliacha kutumia
simu nakuieka pembeni,kisha akaanza kumtazama mama yake aliekuwa akitabasamu
uku akimuangalia kwa jicho la udadisi,lililomfanya mazoea kujishitukia)
Bi masinde:mazoea
unataka kuwa mzigo kwangu si ndio?
Mazoea:samahani mama!
Bi masinde:samahani ya
nini?,
Mazoea: umeniita ..sikukusikia
Bi masinde:mwanangu
mazoea,maisha ni kama msitu mkubwa,na ni kazi sana kujua vilivyo jificha ndani
ya msitu ,bila kuwa mwenyeji wa msitu huo,na kama kila msitu,kuna kila aina ya hatari
na pia kuna vizuri ndani yake,maua na matunda katika miti ya misituni uwa
mazuri na yakuvutia ,uwavutia wanadamu pamoja na wadudu waumao na
kudhuru,unanielewa mazoea?
Mazoea: (kwa
kusita)..hapana mama?
Bi masinde: mwanamke
mzuri asiye na akili ni sawasawa na pete ya dhahabu katika pua ya
nguruwe,mwanangu upendo ni zawadi ya kwanza aliyotupa mungu wetu ,na upendo
hauwezi thibitika bila ya kuonyeshwa mapenzi,lakini mapenzi ni kama maua mazuri
yaliyopo msituni,sio tu vipepeo hupendezwa na maua bali hata nyuki na wadudu
wakali,nimefurai umetambua aina nyingine ya upendo Lakini siwezi nikakuangalia
ukijiingiza katika njia ya upotovu,juzi nimekuona tena ukiwa na Yule
kijana,Yule bodaboda….alie tupeleka kanisani kipindi tuna amia katika huu
mtaa,nimeona jinsi ulivyoukuwa ukiongea nae,nakuomba iwe mwanzo na
mwisho,sitaki nikukute tena ,na uyaache mazoea na yule kijana…...
Mazoea: sawa mama
nimekuelewa
(mazoea alijibu huku
akijisikia aibu,mara simu ya mazoea ikaita,jina likatokea “jack”,
Bi masinde:anaitwa
jack?
Mazoea: ndio
(bi masinde aliinuka na
kuelekea chumbani kwake ambapo shughuli nyingine za nyumbani zikaendelea.)
Scene
2
(baada ya siku mbili
kupita,jack alikuwa ana mawazo sana ,hakuwa tayari kuachana na mazoea,alikuwa
kijiweni akifikiri chakufanya)
Selemani: (rafiki yake
jacky)….oyo naona leo hauko sawa kabisa ,vipi au ndo mambo ya mama zuena tena
Jacky:mama zuena!!?,
aah achana naye,mke wa mtu sumu aisee,yani tangia nikutane na mazoea ,mama
zuena nimeshamsahau kabisa
Sele: duuh!,kile
kigashi cha kilokole,daah we hatari,hadi pale umeshaingia?
Jacky:ah!,bado
sijala,siunajua wale wanapenda mapenzi ya kweli,dah ila mkali
Sele:sasa mawazo ya
nini tena?
Jacky: juzi sikaniambia
anataka asome sijui,mara anaogopa,nimsubiri hadi ndoa,agh!! ,habari ya mapenzi
basi,alafu bi mkubwa wake kagundua naona, maana alipita akanikazia macho
kichizi.
Sele: aaah!.kwani
asomi?,au ndo inshu ya mapenzi na shule na mambo ya bwana yesu hapendi,hahahaha
!, sasa mbona iyo inshu ndogo tu, mtoto
muite geto,mwambie unaumwa akija tu,hucheleweshi, baada ya apo atajijua yeye na
yesu wake.
(jacky akatulia kimya
kidogo,ghafala akatokea bwana masinde ambaye alikuwa akitoka kazini na kutaka
usafiri wa bodaboda hadi kwake,bwana masinde alizoea kutumia usafiri wa jacky
kutokana na uendeshaji mzuri wa jacky., .jacky aliona ndio kapata fursa ya
kumuona mazoea,na safari ikaanza hadi nyumbani)
Bwana masinde:
(alipofika nyumbani,)…mama mazoea!!,mama mazoea!!.
(Aliita bila
mafanikio,)……..mazoea!!,mazoea!!
Mazoea: abee baba
Bwana masinde:njoo
haraka,ulikuwa wapi ,mi naita muda wote?
Mazoea:nilikuwa
najiandaa kuendaa kanisani
(mazoea alishitushwa
baada yakumuona jacky aliyekuwa akimtazama kwa makini sana,kama mtu anaetoa
ishara ya ujumbe usoni)
Bwana masinde: yani leo
hukuenda mitha ya asubuhi na mama
yako?...eeh!!,haya yukwapi mama yako,emu ingiza hii mizigo ndani
Mazoea:sawa baba,mama
ametoka,hajaniaga
Bwana masinde; sasa
atakua ameelekea wapi,nilitaka niongee nae ndo niondoke, na nampigia hapa
hapatikani,
(baada ya mazoea
kupeleka mizigo ya baba yake ndani,anatoka tena nje)
Bwana masinde: sasa
kijana naomba umpeleke mwanangu kanisani,apa mimi itabidi nimsubiri uyu
mwanamke, embu nipe namba yako,napenda sana huduma yako na una heshima kwakweli
(jacky alitabasamu na
kumpatia namba yake mzee masinde,akampakia mazoea,ambaye alikua akionyesha sura
ya wasiwasi,baada ya jacky kuwasha pikipiki alielekea moja kwa moja hadi
nyumbani kwake,wakati wote mazoea alikua akilalamika kuwa anahitaji kuenda
kanisani)
Jacky:mazoea mbona
umebadilika sana,ninakupenda, siwezi ishi bila yako mazoea,
Mazoea:hata mimi
ninakupenda jacky lakini….
Jacky : lakini nini mazoea
(uku akimvuta mkono mazoea waingie ndani)
Mazoea:jacky!!!.hapana
ndani siingii,tuongelee hapahapa na unipeleke kanisani
Jacky:kwanin usiingie
mazoea,mara moja tu
(baada ya jacky
kumlazimisha sana mazoea hatimaye wanaingia ndani ambako mazoea anashawishika
kufanya tendo la kimapenzi kwa mara ya kwanza,)
Scene
3
Baada
ya wiki moja
Jacky:jomba mbona kimya,sioni kitu mezani
Alfred:asee uyu mtoto ulimtoa wapi anaonekana sio
mzoefu wa mambo kabisa
Jacky:aah gashi mmoja wakilokole,vipi sasa iyo video
ushairusha au?,hujanipa mkwanja,sikusomi yani
Alfred:usikonde babu,muda wowote ngoma iko
hewani,mzigo nakutumia sasa ivi
(jacky alichukua rekod ya video ya tendo la faragha alilokuwa akifanya na mazoea na sasa video
ilisambaa mitandaoni baada ya jacky kuiuza kwa wasambazaji wa video za ngono,magazeti ya udaku
yalichapisha nakala yakiwa na kichwa cha habari “AIBU TUPU”,video ilisambaa na
kila mtu akajua,ilikua ni aibu kubwa katika familia ya mzee masinde,)
Bwana masinde: iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni
pa mtu,lakini mwisho wake ni njia ya mauti,hata wakati wa kucheka moyo huwa na
huzuni.
(kanisani pia na shuleni kwa mazoea habari
ilisambaa,mazoea alifadhaika sana na kujiona asiye na thamani katika
jamii,alirudi kwa mama na baba yake akilia baada ya kutoroka kwa kipindi cha
siku mbili kutokana na aibu iliyojaa katika nafsi yake,na mama yake alikua wa
kwanza kutamka neno baada ya kimya cha muda mrefu
Mama masinde:nimekusamehe mwanangu( huku akilia
alimfuata mwanae na kumkumbatia.
mwisho
….
Maoni
Chapisha Maoni