GRIGORY RASPUTTIN
Dunia inamambo mengi ya kutushangaza, waswahili husema ukistaajabu ya musa , basi utayaona ya firauni.
historia inavingi ilivyovificha na kueka wazi yale yanayoweza kuelezeka kwa akili ya binadamu
ukiongelea nchi zinazoongoza kwa ubabe duniani,huezi kuisahau nchi ya urusi..
lakini watu wengi wameijua urusi baada ya vladimir lenin,kiongozi mwenye itikadi za ujamaa , kupindua utawala wa tzar Nicholas II mnamo mwaka 1917,
neno tzar ni sawa na neno mtawala au mfalme kwa lugha ya kiswahili
simulizi hii haina lengo la kumuongelea aliyeleta kikomo cha utawala czar nicholas wa pili .
simulizi hii inalenga kumuongelea mtu ambaye kama angekuepo basi mapinduzi ya urusi yasingefanikiwa..
yaani mbabe vladimir lenin asiyeamini uwepo wa Mungu…asingefanikiwa
grigory rasputtin-.warusi wengi,walijiluza mtoto wa mkulima aliyekosa elimu na mlevi kupindukia asiye na stara ya maneno hata maadili, amewezaje kuachiwa madaraka katika nchi ya kifalme,tena uongozi wa watakatifu wa dhehebu la oxodox
lakini haikua kazi kwa mtu mwenye akili nyingi na miujiza iliyowafanya wanahistoria kukosa jina la kumpa, mtume wa Mungu au mwana wa Shetani aliyekuja kuilaani Urusi
Grigory alizaliwa Siberia mwaka 1869,tangia akiwa mdogo alisemekana kufanya miujiza japo aliishi katika mazingira magumu yaliyomfanya awe mlevi,na muasherati aliyepindukia, mwaka 1904 aliingia kwenye jiji kubwa lenye maendeleo ya kushangaza..saint petersburg, jiji waliloishi koo ya familia za kifalme .
na kama alivyopanga, akafika kwenye kanisa la oxodox ,kwa kudai alikuwa akitimiza maono aliyoonyeshwa na bikra maria
Alipofika kanisani kutoa ushuhuda wake, mgeni huyo akaonekana kama kichaa, hadi aliposogea mbele ya Bishop ,ambaye alikuwa akiaminika zaidi kwenye kanisa la oxodox, Bishop akashika paji la uso Rasputin,kisha akashituka na kupiga magoti chini huku akisema bwana Grigory ni mtu wa Mungu, Grigory Rasputtin akapata umaarufu kwa uwezo wake wa kutabiri,kutambua siri na mawazo ya watu,kuona hata bila kufumbua macho na kuponya watu kwa maombi.
Lakini kuelewa kisa cha grigory rasputin vizuri, inabidi tumjue tzar nicholas ii,mtawala wa urusi,
familia ya kifalme ya urusi ,ilifahamika kama familia ya watakatifu kwakuwa walikuwa waanzilishi wa dhehebu la kanisa la oxodox.
mwaka 1894 ,ulikuwa wakati wa nicholas ii kuiongoza urusi baada ya kifo cha baba yake ,kijana aliyekosa kujiamini kuongoza nchi ya urusi,…..hakua na budi bali kubeba jukumu lisiloepukika
mwaka huo akamuoa bi.alexandra,,kuanzia mwaka 1895 hadi mwaka 1901 alexandra alizaa watoto wa 4 na wote walikuwa wakike,japokuwa aliwapenda watoto wake lakini tzar Nicholas alihitaji mtoto wa kiume ,kwani wanawake wasingeweza kumrithi, na kama asingepata mtoto wa kiume basi ufalme ungerithiwa na ndugu zake,
july 30 ya mwaka 1904, hatimaye Alexandra akazaa mtoto wa kiume
Tsar Nicholas akapata furaha sana hadi kuandika kwenye diary yake kuwa “Mungu amewatembelea”na kwa mbwembwe akamuita Tsarevich alexis,jina lenye maana ya mfalme anayekuja.
Alexis alikuwa kama kiini cha furaha ya wazazi wake na heshima katika falme nzima.
Lakini furaha yao haikudumu kwani baada ya wiki 6, alexis akagundulika kuwa na tatizo lililotishia uhai wake,alitokwa na damu mfululizo,
Dr.Sergei fedorov, Daktari mashuhuri aliyetegemewa urusi , baada ya kumfanyia uchunguzi akagundua kuwa Alexis alikuwa na ugonjwa uitwao HEMOPHILIA.
Hemophilia ni ugonjwa wa kurithi,wazungu wameutafsiri kama a bleeding disorder, ni kazi kuzuia kuvuja kwa damu kwa mtu mwenye ugonjwa huu , tena katika karne ya 20 ,mgonjwa wa hemophilia ni sawa na maiti anayetembea.
Dr fedorov. akamwambia mfalme kuwa mwanae hatokuja kupona ugonjwa huo ,
lakini anatakiwa alindwe asipate kidonda cha aina yoyote , kwani kama damu yake ikianza kutoka wanaweza kumpoteza.
Matumaini ya mwanae kurithi ufalme wake, yakafa ndani ya moyo wa Tsa Nicholas, Baada ya siku hiyo akamtenga mbele ya Uongozi mzima wa Urusi ili asitokee hata mtu mmoja atakayegundua ugonjwa wa mtoto huyo,Tsarevich alexis alikuwa mtoto mwenye usimamizi wa hali ya juu muda wote,.na kwa walioijua siri hiyo waliahidi kwa vifo vyao kutoitangaza.
Miaka kadhaa ikapita,katika kipindi kigumu cha maisha ya Alexis,
Akiwa katika umri mdogo,akapata ajali ya farasi akiwa anacheza,hali yake ilikuwa mbaya,
Dr.Sergei Fedorov akapoteza matumaini ya kuendelea kupigania uhai wa mtoto huyo,
Alizungushiwa kitambaa kizito puani ili kuzuia damu kuendelea kuvuja,akafunikwa mguu wake ulioumia vibaya,
Alikuwa amekwisha poteza fahamu na dakika zake za kuishi zilikuwa zikihesabiwa na wazazi wawili waliopoteza matumaini.
Mzee mmoja aliyehusika na kumhudumia Tsarevich alexis akasema
“namjua mtu wa Mungu anayeweza kuponya”
Kipindi hicho Grigory Rasputtin alikuwa maarufu kwenye jiji la saint Petersburg.. mponyaji anayependa wanawake…mlevi mwenye utani na tamaa isiyozuilikaa,na japokuwa hakuwa handsome lakini ilikuwa kazi kwa mwanamke yoyote kumkataa.
Akaitwa na Mtawala wa urusi,haikuwa mara yake ya kwanza kukutana na Tsa Nicholas II, baadhi ya vitabu vinadai Grigory Rasputin aliwahi kutembelea Ikulu ya Tsa Nicholas mwaka 1906 akiwa na watumishi wengine, Ilikuwa kazi kuchukuliwa maanani lakini alipomshika mtoto huyo mwenye tatizo la Hemophilia aligundua na kuongea kauli tata inayosema “:ataishi miaka mingi”
Milango ya falme ya Tsa Nicholas Ilipofunguliwa na walinzi ,gari la kifahari likamfikisha mtumishi aliyefanana na mtu aliyeweuka akili,..
Mponyaji huyo akafikishwa hadi kwa Tsarevich Alexis..
Alexandra ,mke wa Tsa Nicholas alionekana kumuamini mtu huyo,lakini kwa dr.Sergei pamoja na Tza Nicholas walimuona kama ameenda kuongeza tatizo hasa pale alipoanza kutoa kitambaa kilichowekwa puani kuzuia damu huku akidai alexis anateseseka, lakini na cha ajabu baada ya kumtoa kitambaa hicho damu zilikuwa hazitoki…
Tsa Nicholas akatazamana na Dr.Sergei kwa mshangao lakini hawakuongea neno kwani tatizo la Hemophilia lilikuwa siri.
Rasputin akatoa shuka kubwa lililoficha miguu ya Alexis iliyoteguka, akaishika huku akiomba kwa kutaja jina la Mungu.
Akahamisha maumivu ya mtoto Yule nakuyaeka kwake kama alikuwa na Bluetooth.
Akalia huku akimuita Alexis akitaka aamke,Dr.Sergei aliona kama upumbavu lakini akastaajabu pale Alexis alipofungua macho yake.
Grigory Rasputin aliondoka huku akichechemea,akalipwa pesa kadhaa na Tza Nicholas ,
Kabla ya kuondoka akamwambia Tza Nicholas pamoja na Alexandra kuwa anaweza akamponya Alexis tatizo la Hemophilia kama wakimuamini.
Tza Nicholas na mkewe wakashangaa jinsi siri hiyo ilivyoweza kujulikana na Grigory Rasputin,
Alexandra alitamani mtu huyo aendelee kuepo mahali hapo lakini Tza Nicholas akamruhusu aende akihofia usalama wa mwanae,…
Siku iliyofuata Alexis alikuwa mzima,mguu wake Ulikuwa umepona kabisa,uzima wake na afya ukamstajabisha kila mtu japokuwa hakuna aliyeshangazwa kama Dr.Sergei. aliyesema huyu mtu namfananisha naWizard Merlin au hata Yesu.
Kwa mara ya kwanza katika sherehe kubwa zinazofanyika urusi,familia ya kifalme ikaenda pamoja Tsarevich Alexis,ilikuwa ni mara ya kwanza kwa watu wengi kumuona,
Kila mtu alimshangaa mfalme aliyetegemewa kuja kuiongoza urusi.
Lakini ghafla Hali ya Alexis ikabadilika akiwa mbele za watu, ukubwa watatizo ukadhihirishwa kwa hofu waliyoionyesha mfalme na malkia .
Na kila mtu akataka ajue siri iliyojificha kwenye afya ya mfalme wa badaaye.
Hakukua na kipingamizi bali kumuita tena mtumishi wa Mungu..
Yakiwa majira ya alfajiri,bwana Grigory Rasputin alikuwa kwenye nyumba ya wanawake wanaojiuza, na baada ya kuitwa jina lake na wajumbe wa mfalme , akaitikia kwa kusema kila kitu walichotaka kumwambia…
Safari nyingine ya Rasputin kuingia kwenye hekalu ikaanza,
Watu wakaanza kuzungumza, safari za Rasputin zisizoisha hekaluni zikazua gumzo kwenye ufalme mzima.
Wengi walichukizwa na mtumishi huyo wa Mungu mwenye tabia zinazopingana na sharia za Mungu.
Lakini wanawake wengi wakazidi kumpenda,umaarufu wake ukazidi kuongezeka,
Tabia zake hakuzificha kwa watu,aliziweka hadharani na kusema.Mungu ni upendo, yupo kwa ajili ya kutusamehe,lakini kabla hujaomba msamaha inabidi kwanza ufanye dhambi,
Grigory Rasputin aliamini dhambi na kutubu kunamueka karibu sana mtu na uwepo wa Mungu…
Tabia zake zilimkera sana Tsa Nicholas,hata hivyo alikuwa ndiye mtu pekee aliyeshikilia hatma ya uhai wa mwanae,
Alexandra alimuamini Grigory Rasputin zaidi kuliko mtu yoyote, hadi Mwaka 1912, Tsarevich Alexis akapona.
Urafiki wa mfalme pamoja na mkewe kwa Grigory haukuvunjika katika kipindi kirefu
.
Lakini watu wengi wa urusi walimchukia,viongozi hawakumtaka,kwani Grigory alianza kutoa maamuzi ya nchi yaliyosikilizwa na mfalme,
Hakuwa na elimu ya kidunia lakini Grigory alikuwa na hekima ya kuzaliwa,maono ya mbele na kipawa cha kweli cha Uongozi kisichojificha,
ushauri wake Ulikuwa wa kusikilizwa na kufatishwa kwani endapo usipoufata madhara yake makubwa yalionekana nchini kote
Mwaka 1914,ulikuwa ni mwaka vilipoanza vita vya kwanza vya dunia….
Tsa Nicholas akaingia vitani pamoja na jeshi lake kupigana na Nchi ya Germany huku akimuachia madaraka Malkia Alexandra,ambaye kila shauri lake la maamuzi alimsikiliza Grigory Rasputin.
Ilikuwa wazi usiopingika kuwa bwana Rasputin alikuwa mtu mwenye nguvu zaidi nchini urusi,
Hali ile ikawaaudhi sana ndugu wa familia za ukoo wa mfalme(nobles)
Kwao mkulima hakustahiri kupata nafasi yoyote katika Uongozi..
Njama za kumuua Rasputin zikaanza, na mnamo mwaka 1916 Dec 30…
Bwana mdogo aitwaye felix yusopov anayetoka kwenye koo moja na mfalme akapokea jukumu la kuutoa uhai wa Rasputin Grigory
Bwana huyo alimuita Rasputin majira ya usiku nyumbani kwake kwa kumdanganya kuwa mke wake alikuwa amezidiwa…
Daktari mtaalamu katika kutengeneza sumu akahusishwa,akaandaa sumu hatari zaidi inayoweza kuua kwa sekunde chache na kuieka kwenye keki,
keki moja ilitosha kuutoa uhai wa mtu kwa sekunde kadhaa, lakini bwana felix akaeka sumu kwenye keki nyingi hadi vinywaji..
Kabla ya Rasputin kuenda nyumbani kwa bwana Felix akaandika barua ndefu na kuiacha mezani kwa Malkia Alexandra kisha akaondoka.
Alipofika nyumbani kwa felix , Grigory Rasputin akakaribishwa mvinyo wenye sumu,naye hakuukataa,akakaribishwa keki,naye hakuzikataa, akazila hadi kuzimaliza. Akanywa pombe hadi akalewa..
Bwana Felix akastaajabu sana ,akaamini mtu huyo hakuwa wakawaida, mara zote Felix alikuwa akitoka na kuwafata wenzake waliopanga nae njama , hakuhitaji kuwasimulia kwani sauti ya Grigory ilisikika akiimba nyimbo yenye mashairi yanayosema
“leo ni siku njema ya kufa”
ndipo mmoja wa kiongozi wa urusi alipotoa bunduki na kumkabidhi Felix.
Felix akaingia ndani na kummiminia risas bwana Grigory Rasputin, Risasi moja ya moyo haikumuua, wakampiga risasi nyingi hadi kufanikisha kumuua na kumtupa kwenye bwawa.
Baada ya kupotea kwa Grigory Rasputin ,malkia Alexandra akaamuru upelelezi na msako ufanyike…
Mapolisi wa Urusi wakaingia kwenye msako wa usiku na mchana kuutafuta mwili wa Rasputin,na baadae wakafanikiwa kuupata ukiwa umeganda kwa barafu jirani na mto, inasemekana pembeni na mahali alipokutwa kulikuwa na alama ya msalaba iliyochorwa kwa kidole chenye damu.
Malkia akiwa hekaluni akaona barua iliyoachwa na bwana Grigory kabla ya kufariki.
Kwa ufupi barua ile ilisema
“rafiki yangu alex, mauti yangu yapokaribu kunifika, siwezi kuyakwepa ,hatahivyo kama nikiuliwa na watu wa kawaida nawe utaishi miaka mirefu,lakini kama muuaji atatokea koo ya kifalme basi na laana itawapata , wote mtakufa ….
Maneno ya kirafiki na laana yalikuwa katika barua moja..
Alexandra alibaki katika majonzi pamoja na hofu ,
akajikuta katika mawazo yaliyokatishwa na sauti ya mpelelezi aliyedai kuupata mwili wa Grigory Rasputin.
Swali la kwanza la Malkia lilikuwa ni nani aliyehusika na kifo chake…
Mpelelezi akataja majina na baada ya kusikia jina la Felix Yusopov ,moyo wake ukakita kwa hofu….
Hata hivo akamzika bwana Rasputin kwa heshima…
Lakini Laana ya Grigory Rasputin haikuwa mbali kutokea…
October 1917,Vladimir Lenin akafanya mapinduzi ya utawala wa Tsa Nicholas wapili, na tarahe 16 hadi 17 july 1918 familia nzima ya Tsa Nicholas ,Malkia alexandra ,watoto wake wote wakauawa
na baada ya hapo mauaji ya watu wote wanaotokea koo ya ufalme yakaendelea
laaana ya Grigory Rasputin ikatimia,wanahistoria hudai labda kama Grigory Rasputin angefatishwa na kuaminiwa basi mauaji hayo yasingetokea.
Maoni
Chapisha Maoni