HISTORIA FUPI YA TUNDU LISSU


TUNDULISSU


          Historia Fupi ya Tundulissu 

Maisha ya binadamu yana siri kubwa,wakati kiza kinapoteka dunia,na tumaini la kuona mwanga tena linapokosekana,maisha ya binadamu huendelea…
Yule mswahili aliyesema hakuna kitu chenye roho ngumu kama paka labda alikosea ,kwani historia ya binadamu inamengi ya kutushangaza,
Wengi walistaajabu pale raisi mstaafu wa marekani aitwae Theodore Roosevelt alipopigwa risasi ya ubavuni na kuendelea kutoa hotuba,mwanamziki 50 cent aliyepigwa risasi 9 na kupona, wengi walistaajabu kupona kwa  mwanajeshi wa kimarekani aitwae Mike Day aliyeshambuliwa kwa risasi 27,huku risasi 11 zikipenya sehemu hatari za mwili wake ..
Na labda historia itamkumbuka mtanzania aliyepona baada ya kushambuliwa risasi 38 huku risasi 16 zikipenya mwilini mwake  ,mnamo tarehe 7 septemba ya mwaka 2017.

Hii ni Swahili short stories, na leo nakuletea historisa fupi ya aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la singida mashariki, mgombea uraisi kwa wa chama cha demokrasia na maendeleo,Tundu  Antiphas Mughwai Lissu.


Alizaliwa januari ya tarehe 20 mwaka 1968.na alisoma shule ya msingi Mahambe iliyopo Singida, akiwa shule ya msingi,hakukubali hata mara moja kuamka saa 11 alfajiri kuwahi namba.
Na siku zote alikuwa akigoma kufanya kazi za walimu ikiwemo kulima mashamba yao pamoja na kuwachotea maji..kitu kilichopelekea bakora kwake kuwa kama uji na mgonjwa lakini hakukoma akiamini walimu hawakuwa sahihi.,hata hivyo pamoja na tabia zake zilizowahudhi walimu , pia alisifika sana kwa uwezo mkubwa wa akili darasani

Alipomaliza shule ya msingi akajiunga na masomo ya sekondari baada ya kufaulu vizuri,akaanza masomo yake  katika shule ya ilboru iliyopo mkoani Arusha.
Japokuwa alikuwa mwanafunzi mdogo kuliko wote lakini alikuwa kama mwiba kwa walimu pamoja na viongozi wa shule ambao yeye  alikuwa akiwaita manyoka,kwa kushindwa kutetea wanafunzi wenzao na kupeleka kila taarifa kwa walimu.
Baada ya kufaulu vizuri mtihani wa kidato cha sita,Mwaka 1987 akajiunga na kidato cha 5 katika shule ya sekondari Galanosi iliyopo mkoani Tanga.
Akiwa Galanosi akapewa uenyekiti wa  kamati ya Taaluma,hata hivyo akakorofishana vibaya na walimu wa taaluma na kujikuta akivuliwa cheo hicho.
Katika moja ya tukio linakumbukwa wakati akiwa kidato cha sita,lilihusu sherehe ya mahafari, ambako wanafunzi wa kidato cha sita wakaruhusiwa kucheza na wanafunzi wa shule ya korogwe girls lakini wanafunzi wa kidato cha nne wakakataliwa na kuambiwa wataletewa muziki wa taarabu .
Lissu aliona huo ulikuwa uonevu,naye hakusita kutetea haki aliyoiamini,hivyo akaandika waraka unaosema “Taarab for whose interest”, akimaanisha taarabu kwa maslahi ya nani.
Waraka huo hakuuandika jina ila akaubandika kwenye ubao wa matangazo katika nyakati za usiku.
Walimu walipousoma waraka ule,wakakasirishwa sana ,Hata hivyo hawakuhitaji kusumbua akili zao.wakiamini kulikuwa na mwanafunzi mmoja tu,aliyepinda kiasi cha kufanya maamuzi yale.
Lissu akaitwa mchochezi na kusimamishwa kwa muda kuhudhuria shuleni lakini….baadae alirudishwa shuleni na kufanya mtiani wa kidato cha sita,ambao alifaulu vizuri
Mwaka 1989 alijiunga jeshi la kujenga taifa ,Mafinga (JKT),kisha Itende JKT
Wakati ambapo vuguvugu la vyama vingi likiwa limepamba moto nchini.
Na huko inakumbukwa kuwa aliwahi kujikuta akiingia katika wakati wa sintofahamu baada ya kutumia kauli nzito mbele ya Uongozi,kauli inayosemekana kuwahudhi sana viongozi.
Inasemekana tukio hilo likapelekea kuwa mwisho wake wa kupangiwa kazi , akihisiwa kuwa usalama wa taifa.
Mwaka 1991 alijiunga na kitivo cha sharia katika chuo kikuu cha Dar es salaam.
Huko aliendelea na harakati zake za kupigania haki za wanafunzi,na kujiunga na chama cha NCCR mageuzi,kipindi chama kikiwa chini ya mheshimiwa mrema.
Mwaka 1995 Lissu akaenda kusomea shahada ya uzamili katika chuo cha Warwick kilichopo uingereza, 
Na Mwaka 1997 alirejea na kufanya kazi ya sharia mkoani Arusha. Na baadae akaoa na kuamia Jijini Dar es salaam
Lissu akawa mmoja wa wanasheria katika chama cha wanasheria wa mazingira
Na hapo akaanza harakati za kupigania haki za wanyonge na maliasili za nchi bila woga wowote
mwaka 2004 alijiunga na chama cha demokrasia na maendeleo.
Lissu alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kuwa mtetezi wa haki za wachimbaji wadogo pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo ambako kampuni kubwa za uchimbaji  madini 
Ukiuliza watu wake wakaribu watakuambia lissu ni mtu ambaye siku zote hakuwahi kuwa mpole au kufanya mambo yake kimyakimya.
Historia yake ni ndefu na iliyojaa matukio ambayo mengine unaweza usiamini kama hukushuhudia.
Wanaomjua wanaamini ana nguvu mbili ambazo hakuna shule inayoweza kumfundisha mtu
Ujasiri na umahiri wa kuzungumza….
Mtu mmoja mwenye kuheshimiwa sana,aliwahi kusema….katika kila baya litokalo kwa binadamu pia kuna zuri usilolijua, na ukifanikiwa kulijua litakalokupendeza,   iga….


Maoni